RSS

Jeneza la Kuhani Mkuu Aliyesimamia Hukumu ya Yesu Lagundulika

kayafa

Kayafa alikuwa ni kuhani mkuu wa Wayahudi kuanzia mwaka 27 hadi 36 baada ya Kristo.  Yeye alikuwa ni Sadukayo (Matendo 5:17). Alikuwa ni adui mkubwa wa Yesu Kristo.

Kayafa ndiye aliyetoa pendekezo kwa makuhani na wakuu wengine wa Kiyahudi walikokutana kujadiliana juu ya muujiza wa Bwana Yesu wa kumfufua Lazaro. Imeandikwa:

Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.

Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.

Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote;

wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. (Yohana 11:47-50).

Alikuwa ni Kayafa pia aliyemhoji Bwana Yesu baada ya kukamatwa. Imeandikwa katika Mathayo 26:57-66:

57 Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.

58  Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.

59  Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;

60  wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa uongo wengi.

61  Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.

62  Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?

63  Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

64  Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.

65  Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;

66  mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa.

Baada ya Bwana Yesu kufufuka kwa wafu na kupaa kwenda mbinguni, mitume wake ndio walioendeleza kazi yake ya kueneza Injili ya ufalme wa mbinguni. Kayafa aliendeleza chuki yake hata kwa mitume wa Yesu. Imeandikwa katika Matendo ya Mitume 4:1-6:

1  Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,

2  wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.

3  Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.

4  Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.

5  Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu,

6  na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.

Kuna watu wengi wanaotilia shaka Biblia na hata watu wa dini zingine wanasema kuwa Biblia imepotoshwa.

Mwaka 1990 mabuldoza yalikuwa yakisafisha eneo kwenye sehemu moja kusini mwa Yerusalemu ili kujenga kituo cha michezo ya watoto. Katika uchimbaji ule, jembe la buldoza lilitoboa mahali ambapo kulikuwa na sehemu ya kuzikia wafu ya zamani.

Kazi ilisimama na wataalamu wakaitwa. Wataalamu hao walikuta humo ndani majeneza yam awe (ossuaries). Haya ni majeneza ambayo yalitumika kuhifadhi mifupa ya wafu.

Wayahudi walikuwa na kawaida kwamba mtu akifa, mwili wake huweka kwenye mapango ya makaburi kwa mwaka mzima. Kisha baada ya kuoza na kubakia mifupa tu, mwaka mmoja baadaye wanakuja kufungua kaburi lile na kuweka mifupa yake kwenye hilo jeneza la jiwe. Na baadaye ndugu wengine wa familia wakifa, nao mifupa yao iliwekwa kwenye jeneza hilohilo. Linakuwa ni jeneza la familia.

Jeneza mojawapo katika kaburi hili lilikuwa limepambwa sana kwa michoro mizuri. Juu ya jeneza hilo kuliandikwa jina la Kayafa.

Caiaphas

Wasomi wa mambo ya kale waliochunguza mifupa iliyokuwamo humo wanakubaliana kwamba huyo alikuwa ni Kayafa kuhani.

Unaweza kusoma zaidi HAPA.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on April 7, 2013 in Uncategorized

 

Tags: ,

Farao na Majeshi Yake Walitupwa Bahari ya Shamu

chariot

Biblia inasema kuwa Waisraeli walikaa Misri kwa miaka 430 ndipo Mungu alipowatoa kwa mkono wa Musa. Katika kutoka kwa Misri walitembea kwa miguu kupitia jangwani. Hiyo ilikuwa ni miaka zaidi ya 3000 iliyopita. Lakini Biblia inasema kuwa farao na jeshi lake waliamua kuwafuata Waisraeli ili kwenda kuwarudisha tena Misri, maana waliwaza kuwa sasa wangekosa watu wa kuwafanyia kazi. Imeandikwa:

Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye; tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maakida juu ya magari hayo yote. (Kutoka 14:6-7).

Lakini Mungu aliigawanya Bahari ya Shamu na wana wa Israeli wakapita. Farao na jeshi lake nao waliingia baharini wakati maji yakiwa yamegawanyika. Ndipo wakiwa katikati ya bahari pamoja na magari yao, Bwana akafanya jambo. Imeandikwa:

Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa Bwana anawapigania, kinyume cha Wamisri. (Kutoka 14:25).

Baada ya hapo Bwana alimwambia Musa ainue tena fimbo yake.

Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. (Kutoka 14:27-28).

Sasa swali ni kwamba, je, kuna masalia yoyote hivi leo ya magari hayo ya Wamisri kwenye Bahari ya Shamu?

Mwanaakiolojia maarufu wa mambo ya kibiblia, Ron Wyatt, aliwahi kufanya uchunguzi ili kuweza kugundua mahali ambapo wana wa Israeli walipita wakati wakivuka Bahari ya Shamu. Katika uchunguzi wake, Ron pamoja na wanawe wawili, waliweza kugundua vitu mbalimbali.

Mojawapo ya vitu walivyoona ni magurudumu ya magari ya kukokotwa na farasi yakiwa chini ya bahari. Magurudumu haya, kutokana na kuwapo humo kwa maelfu ya miaka, yalishafunikwa na matumbawe (corals).

Hili ni mojawapo ya magurudumu ambalo limefunikwa kwa dhahabu. Yamkini ndiyo maana liliweza kudumu kwa muda wote huu likiwa bado linaonekana kama jipya.

gurdm

Hili ni gurudumu jingine ambalo limefunikwa kabisa na matumbawe kiasi kwamba halionekani tena. Lakini unapotazama kwa makini unaweza kutambua umbile lake.

gurdm 2

Haya nayo ni magurudumu mengine ambayo yamefunikwa hata zaidi na matumbawe. Hata hivyo, bado pia tunaweza kutambua maumbo yake ya duara na hata ishata ya spoku zake.

gurdm 4

Biblia ni Neno la kweli la Mungu. Kila kitu ilichosema, ni Mungu wa mbinguni amesema. Kwa kuwa Mungu si mwanadamu hata aseme uongo, basi Biblia ni kweli ya Mungu.

Mwamini Yesu maana Yeye ni njia, kweli, na uzima milele yote.

 
2 Comments

Posted by on April 6, 2013 in Uncategorized